Audiopedia Corona Campaign

Je corona ni nini na ninaweza kufanya nini kuhusu Corona?

Je virusi vya Corona ni nini? Na ninaweza kufanya nini kuhusu virusi vya corona?

Virusi vya corona ni vijidudu vidogo (vidogo sana huwezi kuviona kwa macho ya kawaida) ambavyo vinaweza kusambaa na kusababisha magonjwa kwa watu. Virusi vya corona huleta dalili zinazofanana na mafua kama vile kikohozi kikavu, kupumua kwa tabu, homa, na kuumwa kwa mwili.Virusi vya Corona huathiri sana mfumo wa upumuaji. Wakati maambukizi mengine sio ya hatari sana, virusi vya corona vinaweza kusababisha kichomi (maambukizi makubwa ya mapafu) saa zingine huweza kusababisha vifo.

Mtu yeyoye yule anaweza kupata virusi vya Corona. Wakongwe na watu wengine walio na magonjwa mengine, kwa mfano magonjwa ya upumuaji, saratani au kisukari, wapo hatarini zaidi kukabiliwa na athari kali zaidi.

Virusi vya Corona huenezwa kutoka kwa mtu aliyeathirika kupitia kwa matone yanayotoka wakati anapopumua, anapokohoa, au anapopiga chafya na kusambaa kwa watu,kwenye sehemu, au kwenye chakula. Virusi vya corona huingia mwilini kupitia mdomo pua, na macho. Mara tu vinapokuwa mwilini, vinaweza kuongezeka na kuenea katika maeneo mengine. Virusi vya Corona vinaweza kukaa mwilini hadi siku 14 kabla ya dalili za nje kujitokeza. Hivyo, mtu anaweza kuwa na virusi vya corona na asijue, na kueneza virusi hivyo kwa wengine.

Kwa sasa hakuna chanjo au tiba ya corona. Virusi vya corona havitibiwi kwa kutumia dawa za kupunguza uchungu au tiba za nyumbani. Virusi vya corona vinaweza kudhibitiwa kwa kuzuia kuambatana navyo na kuosha mikono kila mara.

Ili kuzuia maambukizi nawa mikono kwa kutumia sabuni na maji. Nawa mikono hata kama huoni uchafu wowote.Nawa mikono yako kwa umakini ukitumia maji na sabuni kwa sekunde 20 hivi,hakikisha umesugua mikono yako upande wa mbele na nyuma na kwa makucha. Hakikisha unanawa mikono yako kabla, baada na wakati wa kuandaa maankuli, baada ya kutoka msaalani,kabla ya kula,wakati wa kuwahudumia wagonjwa, baada ya kuhudumia mifugo au uchafu na kinyesi cha mifugo na baada ya kukohoa,kupiga chafya au kushika mapua.

Usishike macho,pua na mdomo kabla hujanawa mikono. Mikono hushika maeneo tofauti na huweza kupata virusi hivyo. Mikono ikipata viini hivyo , inakuwa rahisi sana kusambaza virusi hivyo kwa macho,pua au mdomo. Hivyo basi virusi hivyo vinaweza kuingia mwilini upesi sana na ukawa mgonjwa.

Ni muhimu kutokaribiana na yeyote yule aliye na joto jingi,aliye na kikohozi au maradhi ya mfumo wa kupumua. Unapokohoa au kupiga chafya, hakikisha umefunga mdomo wako na mapua kwa kutumia upande wa kiwiko au karatasinya sashi. Kisha tupa karatasi hiyo ya sashi uliyotumia. Usiteme mate hadharani.

Dumisha umbali wa mita moja kati yako na yeyote anayekohoa au kupiga chafya. Usimkaribie yeyote yule aliye na joto jingi au anayekohoa.

Ikiwa utahitajika kumshughulikia yeyote yule aliye na joto jingi,anayekohoa au aliye na shida ya kupumua vyema,usisahau kuvaa mask ya kujikinga na jifunze usafi wa mikono.

Ili kuzuia kuambukizwa virusi vya corona, ni vyema kuzuia kukaribiana sana na watu. Virusi vya corona na virusi vingine vinaweza kusambazwa watu wakisalimiana kwa mikono kisha baadaye kugisa macho,mapua na mdomo. Kwa hivyo, unapokutana na watu usiwasalimie kwa mikono,kukumbatiana au kubusiana. Wasalimu watu kwa kuwapungia mkono,kutingisha kichwa au kuinamisha kichwa ishara ya salamu. Ikiwa unakisia kuwa virusi vya corona viko eneo lako, kaa nyumbani ili kuzua kukutana na watu wengine.

Kaa nyumbani ikiwa unajihisi mgonjwa, au ikiwa uko na dalili za kuumwa na kichwa na mafua au homa hadi upone. Ikiwa unapiga chafya, unakohoa , joto jingi mwilini au unashindwa kupumua yema, pata ushauri wa daktari mapema iwezekanavyo kwani hii inaweza kuwa ni maambukizi ya mtumo wa kupumua au matatizo mengine makubwa.

Dhana potovu na uvumi kuhusu virusi vya corona ni hatari sana na hata watu wengine wanauwawa kuhusiana nayo. Kwa mfano kunywa pombe au vinywaji vingine kama pombe vitahatarisha maisha yako badala ya kuzuia virusi vya corona. Hata habari unazopata kutoka kwa marafiki zako au watu wa ukoo yaweza kuwa si sahihi au hatari. Fuatilia habari kutoka kwa wizara ya afya au wahudumu wa afya katika eneo lako.

Unaweza kusaidia kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona kwa kusambaza ujumbe huu. Tafadhali wasambazie marafiki na familia yako ukitumia mtandao kama wa Whatsapp.

Ujumbe huu umeletwa kwako na Audiopedia,mradi wa kimataifa unaosaidia jumbe za afya kusikika. Jifunze zaidi katika tovuti yetu ya www.audiopedia.org