Je mbinu za homoni za upangaji uzazi ziko na madhara yapi

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Je_mbinu_za_homoni_za_upangaji_uzazi_ziko_na_madhara_yapi

Kwa sababu mbinu za homoni huwa na kemikali sawa ambazo mwili wa mwanamke hutengeneza akiwa mjamzito, mambo haya yanaweza kutokea wakati wa miezi michache ya kwanza:

  • kichefuchefu
  • maumivu ya kichwa
  • uvimbe wa matiti
  • kuongeza uzito
  • mabadiliko katika damu kila mwezi

Mara nyingi madhara hubadilika kuwa nafuu baada ya wiki 2 au 3 ya kwanza au miezi. Ikiwa haupati nafuu na yanakukera au kukuhofisha, muone mhudumu wa afya. Anaweza kukusaidia kubadilisha kiwango cha homoni katika mbinu yako au kubadilisha mbinu. Kwa habari zaidi kuhusu madhara maalum ya kawaida kwa kila mbinu ya homoni, soma sehemu zinazoambatana.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020420