Je napaswa kutumia vipi mchanganyiko wa dawa za kupanga uzazi

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Je_napaswa_kutumia_vipi_mchanganyiko_wa_dawa_za_kupanga_uzazi

Vidonge huja katika pakiti iliyo na dawa 21 au 28. Ikiwa uko na pakiti ya dawa za siku 28, meza kidonge kimoja kila siku ya mwezi. Mara utakapomaliza pakiti moja, anza kumeza dawa kutoka kwa pakiti nyingine. (Dawa saba za mwisho katika pakiti ya siku 28 zimetengenezwa na sukari. Hazina homoni ndani. Vidonge hivyo viliyo na sukari hukusaidia ukumbuke kumeza kidonge kimoja kila siku. )

Ikiwa uko na pakiti ya dawa za siku 21, meza kidonge kila siku kwa siku 21, kisha subiri kabla ya kuanza kutumia pakiti nyingine mpya. Damu yako ya mwezi itatoka siku ambazo humezi vidonge. Lakini anza kutumia pakiti mpya hata kama damu yako ya mwezi haijatoka.

Unapotumia pakiti zote mbili ya siku 21 na ya siku 28, meza kidonge cha kwanza siku yako ya kwanza ya hedhi. Ukifanya hivyo utajikinga. Ikiwa ni baada ya siku ya kwanza, unaweza meza kidonge wakati wowote wa siku saba za kwanza za mzunguko wako wa mwezi. Lakini huwezi kujikinga maramoja, kwa hivyo kwa wiki mbili za kwanza unazotumia vidonge unastahili utumie mbinu nyingine ya upangaji uzazi au usishiriki ngono. Jaribu kumeza kidonge chako wakati uo huo kila siku. Inaweza kukusaidia kukumbuka kwamba utakuwa ukianza kutumia pakiti mpya siku io hiyo ya wiki.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020426