Je nawezaje kuzungumza na wazazi wangu

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Je_nawezaje_kuzungumza_na_wazazi_wangu

Wakati mwingine huwa ni vigumu kuzungumza na mama au baba yako. Wazazi wako wangependa uishi kitamaduni, lakini unahisi kuwa nyakati zimebadilika. Unaweza kuhisi kuwa wazazi wako hawakusikilizi au hwakuelewi. Au unahofia kuwa watakasirika.

Familia yako inaweza kukupenda bila ya kukubaliana na kila unachosema. Wakati mwingine watakasirika kwa sababu wanakujali - sio ati hawakupendi. Jaribu kuzungumza nao kwa heshima na uwasadie kukuelewa.

Kwa mawasiliano bora:

  • Chagua wakati mzuri wa kuzungumza, wakati wazazi wako hawana shughuli, wamechoka au wana wasiwasi kuhusu jambo fulani.
  • Zungumza nao kuhusu mambo yanayokupa wasiwasi na malengo yako. Waulize wangefanya nini.
  • Ili uweze kuanzisha mazungumzo, wape kitu cha kusoma au waonyehse picha. Unaweza kusoma sehemu ya kitabu pamoja ikiwa inahusiana na shida uliyo nayo.
  • Jaribu usipaaze sauti yako ikiwa utakasirika. Unaweza kuwakasirisha wazazi wako na kuwafanya wafikiri kuwa hauwaheshimu.
  • Ikiwa umejaribu mambo haya yote na bado umeshindwa kuzungumza na wazazi wako, tafuta mtu mwingine ambaye unaweza kuzungumza naye. Inaweza kuwa ni mwalimu, mama ya rafiki yako, shangazi au dadako mkubwa, nyanya, mshiriki pale kanisani au mhudumu wa afya.



Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020820