Je ninapaswa kufahamu nini kuhusiana na kujiua

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Je_ninapaswa_kufahamu_nini_kuhusiana_na_kujiua

Kitendo cha kujitoa uhai kwa kukusudia sababu ya kutotaka kuishi kinaitwa kujiua. Imekadiriwa kwamba vifo vya takriban watu milioni moja ulimwenguni kila mwaka huhusishwa na kujiua.

Hii inamaanisha kwamba kwa kila sekunde 40 ulimwenguni, mtu hujiua. Kadhalika, kuna visa milioni 20 vya kujiua kila mwaka vinavyotibuka na idadi hiyo inaongezeka.

Ni vigumu kupata idadi kamili ya visa hivyo kwani familia nyingi huficha maana kamili ya vifo vinavyosabishwa na kujiua, kwa kuhofia kudhulumiwa na polisi na wanainchi.

Huku visa vya kujiua vinapopungua kwa nchi zilizoendelea, visa hivyo vinaongezeka kwa idadi ya kushangaza kwa nchi zinazoendelea kustawi.

Sababu zinazoaminika kusababisha kujiua ni:

  • Umasikini
  • Kiwango cha chini cha elimu(kisha baadaye kukosa ajira)poor education
  • Kuchipuka kwa kampuni (na kusababisha kupoteza kazi za mikono)
  • Kiwango cha chini cha huduma za afya( Kuadimika kwa wauguzi wanaoelimisha watu kuzuia msongomano wa mawazo)
  • Itikadi za kale na ukosefu wa kufahamu(Watu wanaweza kutokubaliwa katika jamii au nchi kutokana na kufuata itakadi za kale za jamii au nchi fulani)
Sources
  • Felicitas Heyne, Psychologist
  • Audiopedia ID: sw020902