Jinsi gani mbinu za homoni za upangaji uzazi hufanya kazi

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Jinsi_gani_mbinu_za_homoni_za_upangaji_uzazi_hufanya_kazi

Mbinu hizi ziko na homoni, iitwayo estrogen na progestin, ambazo ni sawa na estrogen na progesterone ambayo mwanamke hutengeneza katika mwili wake. Mbinu za homoni ni: 
  • Vidonge, ambavyo mwanamke humeza kila siku.
  • Sindano, ambayo hupewa kila baada ya miezi michache.
  • Implants, ambayo huwekwa katika mkono wa mwanamke na hukaa kwa miaka kadhaa.

Mwanamke hudhibiti mbinu za homoni na huweza kutumika bila ya mwanamume kujua.

MUHIMU! Mbinu za homoni hazizuii dhidi ya magonjwa ya zinaa au VVU.

Mbinu za homoni hufanya kazi kwa kuzuia ovari za mwanamke kutoa yai. Homoni hiyo pia hutengeneza kamasi katika mdomo wa tumbo nene sana, ambayo husaidia kuzuia shahawa kuingia ndani ya tumbo la uzazi.

Nyingi ya vidonge vya upangaji uzazi na baadhi ya sindano huwa na estrogen na progestin. Hizi huitwa 'mchanganyiko' wa vidonge au sindano. Homoni hizo mbili hufanya kazi kwa pamoja ili kutoa kinga bora dhidi ya mimba. Hata hivyo, baadhi ya wanawake hawastahili kutumia vidonge au sindano iliyo na estrogen kwa sababu za kiafya, au kwa sababu ya kunyonyesha.

Vidonge vya Progestin-tu (pia huitwa mini-pills), implants, na baadhi ya sindano huwa tu na homoni moja-- progestin. Mbinu hizi ni salama zaidi kuliko dawa zilizochanganywa au sindano kwa wanawake ambao hawastahili kutumia estrogen, au wanaonyonyesha.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020418