Kila mtoto anastahili chanjo

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Kila_mtoto_anastahili_chanjo

Wazazi wengi hukosa kumpeleka mtoto kupokea chanjo eti kwa sababu mtoto ana homa, kikohozi, mafua, kuharisha au maradhi mengine. Chanjo hata hivyo ni salama kwa mtoto anaye uguwa maradhi madogo madogo.

Pia ni salama kuumpa chanjo mtoto ambaye ni mlemavu au ana utapiamlo. Kama mtoto anavyo virusi vya ukimwi au anashukiwa kuwa na virusi hivyo, mhudumu wa afya aliye hitimu atashauri ni chanjo zipi ambazo mtoto huyo anaweza kupokea.

Baada ya chanjo, mtoto anaweza kupata joto jingi mwilini, upele au kidonda kidogo mahali alipodungwa kwa shindano. Haya yote ni kawaida na huwa ni ishara kuwa chanjo inafanya kazi mwilini. Watoto walio chini ya miezi sita wanastahili kunyonya zaidi kwa muda baada ya kupokea chanjo; watoto walio zaidi ya miezi sita wanapaswa kula na kunywa zaidi. Ikiwa mtoto atazidisha joto mwilini hadi zaidi ya selsias thelathini na nane, peleka mtoto huyo katika kituo cha afya au kwa muhudumu wa afya.

Maradhi ya surua ni hatari zaidi kwa watoto walio na utapiamlo kwa hivyo wanastahili kupokea chanjo dhidi ya surua haswa kama utapiamlo ni kali.

Sources