Kuna umuhimu gani kwa wazazi kufikiria kuhusu kuzuia watoto kuumia

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Kuna_umuhimu_gani_kwa_wazazi_kufikiria_kuhusu_kuzuia_watoto_kuumia

Kila mwaka, takribani watoto milioni 1 hufa kutokana na majeraha. Makumi ya mamilioni wengine huhitaji kukaa hospitalini kwa sababu ya majeraha madogo. Wengi huachwa na ulemavu au uharibifu wa ubongo.

Majeraha huathiri watoto wa kila umri. Wasichana na wavulana wa chini ya umri wa miaka 5 wamo hatarini. Wavulana wengi hufa kutokana na majeraha kuliko wasichana.

Ajali nyingi huwa ni zile za barabarani, wakati mwingine hatari ya kufa maji, kuungua, kuanguka na kufa kutokana na sumu.

Ajali za barabarani na kufa maji ndio ajali zinazoongoza katika vyanzo vya vifo.

Mahali ambapo watoto hupata majeraha sana huwa ni nyumbani.

Takribani majeraha yote yanaweza kuepukwa.

Ni wajibu wa familia, jamii na serikali kuhakikisha kuwa haki za watoto kuwa katika mazingira salama zimefuatwa na watoto wamelindwa kutokana na ajali.

Sources