Kwa nini nitafute usaidizi nikihisi kujitoa uhai

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Kwa_nini_nitafute_usaidizi_nikihisi_kujitoa_uhai

Usaidizi na uhusiano wa nguvu ni nguzo muhimu zitulindazo kwa afya ya akili. Wanaotaka kujiua huwa wanihisi upweke. Unaweza kuwa na mpenzi, familia na marafiki wengi, lakini bado ujihisi mpweke. Kuwa na watu kati yetu haimaanishi kuwa tumeungana nao. Ikiwa uko na mawazo ya kujiua, waweza kufikiria ya kwamba hakuna mtu atakayekuelewa au kukusaidia. Lakini sivyo.

Kukutana na wanawake wengine kunaweza kukupa nguvu, ambayo itakayokusaidia kukabiliana na shida zako za kila siku. Dunia ni ndogo. Kwa kuzungumza na wengine, watu huanza kujua ya kwamba wengi wao hupitia shida zizo hizo. Hii huwasaidia kupunguza mzigo na huwasaidia kutambua kiini husika cha shida.

Kando na hayo, ni rahisi kupata majibu ya shida kwa kuzungumzia shida hizo katika kikundi au na wanawake wengine. Mmoja wa wanawake anaweza kuwa na wazo ambalo hukufikiria hapo awali la kubadili jambo unalopitia. Vivyo hivyo wewe pia unaweza kuwa na wazo litakalosaidia mwingine.

Wakati mwingine, wanawake huficha hisia zao (au hawatambui kuwa wanazo), kwa sababu wanafikiria au hufunzwa ya kwamba hisia zingine ni mbaya, hatari au za aibu. Kwa kusikia wengine wakiongea kuhusu hisia hizi kunaweza kumfanya mwanamke atambue za kwake. Wanawake wengine wanaweza kukusaidia na mawazo, ndiposa hutafanya uamuzi wa haraka usio wa busara bila ya kufikiria vyema. Hii huitwa usaidizi wa hisia na muhimu ikiwa unahisi kujitoa uhai.

Sources
  • Felicitas Heyne, Psychologist
  • Audiopedia ID: sw020914