Kwa nini sistahili kujiua ninapohisi shinikizo la kujiua

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Kwa_nini_sistahili_kujiua_ninapohisi_shinikizo_la_kujiua

Kujitoa uhai na majaribio ya kujiua hutokana na shinikizo la hisia la kutaka kujiua. Yaani, watu wawa hawa hawangelijaribu kujiua siku chache kabla au baada, au kama wangelifikira vyema matendo yao. Hebu fikiria, ikiwa jambo unalopitia laweza kubadilika kuwa bora katika masaa 24 yajayo au wiki lijalo? Je, Huta juta kuwa hai kufurahia hayo?

Jipe nafasi. Jiambie, "nitasubiri masaa mengine 24 (au hata wiki moja) kabla ya kufanya jambo lolote. " Weka nafasi ya mbali kati ya mawazo ya kujitoa uhai na kujitoa uhai, hata kama ni kwa masaa 24.

Ikiwa njia za kujitoa uhai tayari zimo nyumbani mwako(kwa mfano bunduki au sumu), muite rafiki au mtu aliyekaribu na wewe akusaidie kuziondoa. Zinastahili ziwe mbali na wewe au mahali huwezi kuzifikia angalau kwa masaa 24. Unaweza kupeana silaha yako kwa rafiki yako na umwambie asikurudishie kwa angalau masaa 24, hata kama kuna jambo gani. Wakati huu, usiende mahali popote pale palipo na hatari ambapo panaweza kukushinikiza kujiua (kama mashimo makubwa, majengo makubwa, daraja, au kwa reli. Na sehemu zingine kama hizo).

Usinywe vileo au madawa unapohisi kujiua. Japo yaweza kuwa njia ya haraka ya kupunguza uchungu, vileo na madawa vitapunguza shinikizo lako na kukuweka katika hatari ya kujiua bila kufikiria.


Sources
  • Felicitas Heyne, Psychologist
  • Audiopedia ID: sw020915