Mbinu ya kamasi ya upangaji uzazi hufanya kazi vipi

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Mbinu_ya_kamasi_ya_upangaji_uzazi_hufanya_kazi_vipi

Ili kutumia mbinu ya kamasi, sharti uwe makini kuangalia kamasi (majimaji) katika uke wako. Mwili wako hutoa kamasi ya maji maji wakati mwili unapokuwa tayari kushika mimba ili kusaidia shahawa kuingia kwa tumbo la uzazi. Kwa hivyo ikiwa utaangalia kamasi hilo kila siku, utajuwa lini mwili wako utakuwa tayari kushika mimba. Kisha unaweza kutojihususha na tendo la ngono kwa kipindi hicho.

Jinsi ya kugundua ikiwa mwili uko tayari kushika mimba:

(1) Panguza sehemu ya nje ya uke wako ukitumia kidole, karatasi au kitambaa.

(2) Ikiwa kamasi ipo hapo, paka kidogo katikati ya vidole vyako. Iko vipi? Majimaji na yateleza? Kavu na ya kuganda?

Kamasi inayoonekana kwa urahisi, majimaji, na telezi = Mwili uko tayari kushika mimba. Kamasi nyeupe, kavu na ya kuganda = Mwili hauko tayari kushika mimba.


Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020509