Mbona chanjo ni muhimu

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Mbona_chanjo_ni_muhimu

Kila mwaka, takribani watoto milioni moja nukta nne hufa kutokana na maradhi yanayo weza kuzuiwa kwa kutumia chanjo.

Chanjo hukinga mtoto dhidi ya magonjwa hatari ya utotoni. Watoto wote hata wale walio na ulemavu tofauti, wanastahili chanjo. Chanjo hupewa mtoto kwa kupitia shindano au kwa kutiwa kinywani. Chanjo humkinga mtoto dhidi ya magonjwa kwa kuimarisha kinga msingi mwilini. Chanjo humfaidi mtoto tu anapoipata kabla ya maradhi kumvamia.

Mtoto ambaye hajapata chanjo kamili anaweza kuugua surua, kifaduro na magonjwa mengine mengi yanayo sababisha kifo. Watoto wanaosalimika kifo kutokana na maradhi haya hukuwa wakiwa dhaifu. Waweza kulemaza au hata kufa baadaye kwa sababu ya utapiamlo na maradhi mengineyo.

Watoto wanaopokea chanjo kamili hupata kinga dhidi ya maradhi hatari ambayo husababisha ulemavu au hata kifo. Ni haki kwa kila mtoto kupokea chanjo kwa wakati unaofaa.

Kila mtoto, awe wa kike au kiume, anahitaji chanjo kamili. Kinga ya mapema ni muhimu. Chanjo zote zinazoashiriwa kwa watoto chini ya umri wa mwaka mmoja na hata za mwaka wa pili wa mtoto ni muhimu zaidi. Pia inastahili sana kwa mama mja mzito kupokea chanjo dhidi ya pepopunda ili kujikinga mwenyewe na mwanaye.

Sources