Mbona niamini hisia zangu

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Mbona_niamini_hisia_zangu

Wanawake wengi hufundishwa wakiwa wachanga jinsi ya kuwa wakarimu na kujaribu kutomkosea mtu yeyote.

Kwa hivyo, mtu akifanya jambo ambalo humfanya mwanamke kuwa na wakati mgumu/wasiwasi, mara nyingi huwa na wakati mgumu kufanya jambo kutokana na hisia zake.

Lakini kuwa mwangalifu ikiwa:-

  • Utahisi kuwa kuna shida mahali.
  • Utahisi woga au kutaka kuondoka.
  • Hutahisi vyema na maoni au mapendekezo yanayotolewa na mtu fulani.
  • Hutafurahishwa na anavyojiwasilisha kimwili.

Inaweza kuwa vigumu kufanya uamuzi wako kutokana na hisia hizi kwa sababu unaweza kuogopa vile watu wengine watakavyofikiria. Kwa kuongezea hayo, ikiwa unamjua au kumjali mtu huyo unaweza kutokubali kuwa anaweza kukudhuru. Lakini ni vyema uamini hisia zako na uachane na hali yoyote ile ambayo haikuridhishi kabla ya jambo baya kufanyika.

Amini hisia zako. Ni vyema kumkosea mtu ikiwa una makosa kuliko kubakwa.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020308