Mbona wanawake wengine huavyaa mimba

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Mbona_wanawake_wengine_huavyaa_mimba

Sio jambo rahisi kuamua kuavyaa mimba. Baadhi ya dini hufundisha kuwa ni vibaya kuavyaa mimba, na katika mataifa mengi kuavyaa mimba sio salam wala halali. Kuna sababu nyingi ambazo mwanamke atajaribu kuavyaa mimba. Hapa kuna mifano:

  • Ana idadi ya watoto ambao anaweza kuwalea.
  • Uja uzito ni hatari kwa afya na maisha yake.
  • Hana mpenzi wa kumsaidia kumlea mtoto.
  • Anataka kumaliza shule.
  • Hataki watoto.
  • Alishika mimba baada ya kulazimishwa kushiriki ngono.
  • Kuna mtu anamlazimisha kuavyaa mimba.
  • Moto atazaliwa na ulemavu.
  • Ana virusi vya HIV au UKIMWI.

Uja uzito ambao haujapangwahufanyika wakati ambapo:

... mwanamke na mpenzi wake hawajui jinsi uja uzito hufanyika. ... wahudumu wa afya hudhani kuwa wanawake wengine ni wachanga sana kutumia njia za kupanga uzazi. ... wanawake hulazimishwa kushiriki ngono. ... mbinu za kupanga uzazi hazipatikani, hazitumiki vizuri au hazifanyi kazi.

MUHIMU: Mwanamke ambaye ameshirkingono katika muda wa siku 3 zilizopita anaweza kuzuia kushika mimba ikiwa atafanya mambo haraka.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020203