Migogoro ipi ya kawaida inayohusisha mashemeji

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Migogoro_ipi_ya_kawaida_inayohusisha_mashemeji

Katika nchi nyingi, mwanamke anapoolewa hutarajiwa kuondoka alikozaliwa na kwenda kuishi na familia ya mumeo.

Kwa wanawake wengi wachanga jambo hili huwafanya wateseke kwa sababu huwapesa wazazi na ndugu zake na kufanya ahisi upweke, kutengwa, na bila msaada kutoka kwa familia ya mumeo.

Umaskini, mila na tamaduni katika nchi zinazoendelea hufanya familia kuishi kwa pamoja katika nyumba moja na hii husababisha wanadoa waliooana karibuni kulazimishwa kuishi kulingana na itikadi na tamaduni za wazazi na babu zao.

Katika hali hii, mashemeji wanaweza kufanya maisha kuwa magumu kwa msichana aliyeolewa na wanaweza kuingilia uhusiano wake na mumeo. Mifano halisia ya kuingiliwa kwa uhusiano na mashemeji zinazoweza kushuhudiwa ni:-

  • Mwanamke aliyeolewa atahitajika kuwasaidia mashemeji sana na kuwashughulikia ikiwa watakuwa na mahitaji fulani.
  • Mashemeji wanaweza kutokubali uhusiano huo na kukosa kumtunza mkwe vyema.
  • Mashemeji wanaweza kumshinikiza mkwe wakati atakosa kuzaa watoto wa kiume katika familia au ikiwa hatakuwa na ajira.
  • Ikiwa nyumba ya familia ya mume wanayoishi na ambayo bibi ameletwa ni ndogo basi mashemeji wanaweza kumpa bibi huyo chakula kidogo na kumnyima vitu vingine muhimu kwa sababu hawataki kutumia pesa nyingi kwa ajili ya kumtunza huyo bibi.
  • Mashemeji wanaweza kosa kumtunza au kumnyanyasa mkwe wao kwa ;
  • Kumnyanyasa na kumtusi au kumfanyia mzaha kwa kumsengenya.
  • Kumshambulia
  • Kumnyima chakula.
  • Kwa kumkataza kwenda nje kukutana na mtu yeyote
  • kwa kumkataza kuwatembelea wazazi wake
  • Kwa kutomruhusu kuzungumza na wageni waliotembelea familia yao.
  • Kwa kumkataza kuwaona watoto wake.


Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw021015