Migogoro ipi ya kawaida inayohusishwa na kazi za nyumbani

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Migogoro_ipi_ya_kawaida_inayohusishwa_na_kazi_za_nyumbani

Katika nchi nyingi, wanawake huwa na jukumu la kufanya kazi za nyumbani kulingana na tamaduni zao.

Wanawake huwatunza waume, wazazi na watu wa ukoo, watoto, wagonjwa na wazee wao. Hutafuta kuni na maji ya kunywa, hupika na kuosha, hufanya usafi, kulima na kwa kawaida huwatunza wanyama walio nao.

Ukosefu wa vifaa vya kuwatunza watoto na huduma za kuwasaidia katika maeneo tofauti ulimwenguni humaanisha kutunza familia, kuongezea kwa kazi zile zingine za nyumbani kunaweza kuchukuwa muda mwingi wa mwanamke na kunaweza kupunguza uwezo wa mwanamke kutafuta ajira.

Kazi hizi za nyumbani zinaweza kuwa mzigo mkubwa kwa mwanamke aliye na nguvu na afya yuko na siku nzima kushughulika kazi hizo. Kazi hizi zinaweza kumkosesha mwanamke kufanya kazi ya mapato na wingi wa kazi hizo kunaweza kumfanya mwanamke kushindwa kufanya kazi hizo ikiwa yeye ni mnyonge au akigonjeka.

Wakati wanawake wanapoomba msaada kutoka kwa waume wao kwa kawaida hukosa msaada kwa minajili ya kwamba kazi za nyumbani zinajulikana kuwa ni "kazi ya mwanamke"-hata kama mwanamke hufanya kazi ya kuajiriwa ili kusaidia familia yake kimapato.

Takwimu zinaonyesha kwamba wanawake walioko katika nchi zinazoendelea kukuwa, kwa wastani, hutumia masaa matatu kwa siku zaidi ya waume kwa kazi zisizolipa kama kazi za nyumbani na kuwatunza watoto na wazee. Takwimu hizo zinaonyesha pia kwamba wanawake walio na watoto wadogo wengi huweza kosa kutimiza majukumu yao yote kwa muda unaofaa.

Aidha katika nchi nyingi wanawake huwajibika kwa kufanya shughuli za nyumbani, kuwalea watoto na kutoa huduma za kimsingi, huwa na ushawashi mdogo kwa uamuzi wa maswala au matumizi ya nyumbani na huwa wanahisi kutokuhusishwa kwa maamuzi.

Mara kwa mara mzigo wa shughuli za nyumbani na wa kuwalea watoto huwaangukia wanawake ilihali maamuzi muhimu hufanywa haswa na waume, ambayo sio sawa kabisa na yaweza kuleta mafarakano au shida kati ya wanandoa.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw021007