Nafaa kujua nini kuhusu kondomu za wanawake kondomu za wanawake

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Nafaa_kujua_nini_kuhusu_kondomu_za_wanawake_kondomu_za_wanawake

Kondomu ya mwanamke, ambayo hutoshea ndani ya uke na hufunika midomo/sehemu ya nje ya uke, yaweza kuwekwa ndani ya uke wakati wowote kabla ya ngono. Ni lazima itumike mara moja tu, kwa sababu yaweza kupasuka ikiwa itatumika tena. Lakini ikiwa hauna kondomu nyingine yoyote, unaweza kuisafisha na kuitumia tena hadi mara 5. Kondomu ya mwanamke haipaswi kutumiwa kwa pamoja na kondomu ya mwanamume.

Kondomu za wanawake ni kubwa kuliko kondomu za wanaume na si rahisi kupasuka. Hutumika vyema wakati mwanamume huwa juu na mwanamke chini wakati wa kujamiiana.

Kondomu ya mwanamke ni ya ufanisi mkubwa katika mbinu zinazodhibitiwa na wanawake kwa kujikinga dhidi ya mimba na magonjwa ya zinaa kwa pamoja na VVU. Kuna aina 3 za kondomu za kike zinazopatikana. Zile ambazo ni za kisasa ni ghali kidogo. Kondomu aina ya VA hutoshea vizuri kwa mwili wa mwanamke, na huwa haitoi kelele nyingi.

Kondomu za wanawake zinapatikana katika maeneo machache sasa. Ikiwa watu wa kutosha watahitaji mbinu hii, mipango zaidi itawezesha ipatikane.



Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020412