Nafaa kujua nini kuhusu spermicide Mbinu ya upangaji uzazi ya povu vidonge jelly au cream

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Nafaa_kujua_nini_kuhusu_spermicide_Mbinu_ya_upangaji_uzazi_ya_povu_vidonge_jelly_au_cream

Spermicide huja katika aina nyingi--povu, vidonge, na cream au jelly-na huwekwa katika uke kabla tu kujamiiana. Spermicide huua shahawa ya mwanamume kabla ya kuingia ndani ya tumbo la uzazi.

Ikiwa itatumika pekee yake, haitakuwa na ufanisi mkubwa ikilinganishwa na mbinu zingine. Lakini ni muhimu inapotumika kama kinga ya ziada itumikapo na mbinu nyingine, kama diaphragm au kondomu. 

Spermicides zinaweza kununuliwa katika maduka ya dawa na sokoni. Wanawake wengine huwashwa na kujikuna katika uke sababu ya kutumia aina zingine za spermicides.

Spermicides hazina kinga dhidi ya magonjwa ya zinaa yoyote. Kwa sababu spermicides yaweza kuwasha kuta za uke, zinaweza kusababisha vidonda vidogo ambavyo vinaweza kupitisha virusi vya ukimwi kwa urahisi ndani ya damu.

Wakati wa kuingiza spermicide:

Vidonge au dawa zinazosaidia vidonge vyastahili kuwekwa ndani ya uke dakika 10 hadi 15 kabla ya kujamiiana. Povu, jelly, au cream hufanya kazi vyema ikiwa vitawekwa ndani ya uke kabla ya kujamiiana.

Ikiwa zaidi ya saa moja kupita kabla ya kujamiiana, ongeza spermicide zaidi. Ongeza kidonge kipya, dawa inayosaidia kidonge, applicator ya povu, jelly, au cream kila wakati unaposhiriki ngono.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020416