Nafaa kujua nini kuhusu ubakaji uliofanywa na mtu nisiyemjua

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Nafaa_kujua_nini_kuhusu_ubakaji_uliofanywa_na_mtu_nisiyemjua

Watu wengi hufikiria aina hii ya unyanyasaji wa kijinsia wanaposikia neno 'ubakaji'. Mwanamke anaweza kuwa barabarani au kushambuliwa nyumbani kwake. Aina hii ya ubakaji huogopesha, lakini si ya kawaida sana ikilinganishwa na ubakaji wa mtu unayemjua.

Ubakaji wa kikundi.

Mwanamke anaweza kubakwa na zaidi ya mwanamume mmoja. Wakati mwingine mwanamume huanza kumbaka mwanamke na wanaume wengine huona kisha wanajiunga kufanya tendo hilo. Au wakati mwingine wavulana hujumuika na kumbaka mwanamke kuonyesha 'uume' wao kwa wenzao.

Ubakaji wa gerezani.

Wanawake wengi hubakwa na polisi au walinzi wa magereza baada ya kukamatwa. Ubakaji, pia, ni jambo la kawaida kati ya wafungwa wa kiume kama njia ya kuonyesha aliye na mamlaka zaidi. 

Vita.

Askari au wapiganaji hutumia ubakaji kuwatishia/kuwaogofya wanawake na jamii yao, na kuwaaibisha watu. Askari wanaweza kuwabaka wanawake na wasichana wakipokezana mbele ya familia zao kuonyesha mamlaka ya adui.

Wanawake wanaweza kuwekwa katika makambi, na kulazimishwa kufanya ukahaba au kuwa watumwa wa ngono ndiposa waishi, wawalinde watoto wao, au wapate chakula.

Ubakaji ni aina ya mateso unapotumika vitani.

MUHIMU: Wanaobakwa vitani huhitaji kutunzwa vyema /kwa hali ya juu. Anaweza kuhitaji upasuaji kwa sababu ya kuharibika sana sehemu ya siri. Ikiwa mwanamke atapata mimba, yeye na mtoto wanaweza kuteseka kutokana na kumbukumbu za kubakwa na adui.


Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020306