Nahitaji kufanya nini ili niweze kushinda hisia za kubakwa
From Audiopedia - Accessible Learning for All
QR for this page
Unaweza fadhaika kwa muda baada ya kubakwa hata kama mwili wako umepona. Hizi hapa ndizo baadhi ya hisia na maswali mtu hujiuliza.
Ni muhimu mwanamke aliyebakwa azungumze na mtu mwingine au afanye kitu ambacho kitamsaidia ahisi nafuu baada ya kubakwa- kila mwanamke anahitaji kutafuta njia yake mwenyewe itakayomsaidia kupona.
Kwa wanawake wengine, yabidi wafanyiwa matambiko, ilihali wengine hujikaza ili waweze kuwaadhibu wabakaji, au kuhakikisha kwamba wamewakinga wanawake wengine kubakwa. Lolote ufanyalo, kuwa na subira na uwasihi wenzako pia wawe na subira.
Inaweza kuchukua muda kabla uhisi nafuu, lakini unapozungumza na mtu unayemwamini au mwathiriwa yaweza kukusaidia kupona.