Nani hapaswi kumeza dawa iliyochanganywa

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Nani_hapaswi_kumeza_dawa_iliyochanganywa

Wanawake wengine wako na matatizo ya kiafya yanayofanya kuwa hatari kwao kutumia kidonge.

USIWAHI kumeza kidonge ikiwa uko na matatizo yaliyoorodheshwa hapa au ikiwa:

  • Uko na ugonjwa wa ini hepatitis, au macho na ngozi yako yana rangi ya njano.
  • Umewahi kuwa na dalili za kiharusi, kupooza, au ugonjwa wa moyo.
  • Umewahi kuwa na tone la damu lililoganda katika mishipa ya miguu yako, au katika mapafu yako au ubongo.

Mishipa ya varicose kwa kawaida si tatizo, isipokuwa ionyeshe rangi nyekundu na kidonda.

Ikiwa uko na matatizo yoyote haya ya afya, jaribu kutumia mbinu nyingine isipokuwa vidonge vilivyochanganywa vya kupanga uzazi. Lakini ikiwa huwezi, ni bora umeze kidonge kilichochanganywa kuliko kupata mimba.

Jaribu kutomeza dawa iliyochanganywa ikiwa:

  • Unanyonyesha, hakikisha umesubiri hadi pale maziwa yako yanatoka vizuri kabla ya kuanza kutumia dawa iliyochanganywa. Hii kawaida huchukua wiki 3.
  • Unavuta moshi na uko na umri wa zaidi ya miaka 35. Uko na nafasi kubwa ya kuwa na kiharusi au mshtuko wa moyo ikiwa utatumia dawa iliyochanganywa.
  • Uko na ugonjwa wa kisukari au kifafa. Ikiwa unatumia dawa ya kifafa iitwayo ( "fits"), utahitaji kumeza kidonge kilicho na nguvu kilichochanganywa na (mikrogram 50 ya estrogen) ya kupanga uzazi. Pata ushauri wa daktari kutoka kwa mhudumu wa afya au daktari.
  • Uko na shinikizo la damu (zaidi ya 140/90). Ikiwa umewahi kuambiwa uko na shinikizo la damu au unafikiri unaweza kuwa nalo kapimwe shinikizo lako la damu na mhudumu wa afya. Ikiwa wewe ni mzito sana, na hupata maumivu ya kichwa mara kwa mara, kuishiwa na pumzi kwa urahisi, kujihisi mnyonge au kizunguzungu mara nyingi, au kuhisi maumivu katika bega la kushoto au kifua, unapaswa kupimwa shinikizo la damu.
Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020423