Napaswa kufanya nini ikiwa nimebakwa

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Napaswa_kufanya_nini_ikiwa_nimebakwa

Kila mwanamke aliyebakwa yuko na hadithi yake. Lakini kuna vitu kadhaa unapaswa kufanya ili uweze kupona.

Kwanza jiulize maswali yafuatayo:

  • Ni Nani unaweza kumuuliza akusaidie?
  • Je, Unataka kueleza polisi kuhusu kubakwa?
  • Waweza kwenda wapi kwa huduma ya matibabu?
  • Unataka kumwadhibu mbakaji?
  • Unahitaji kuzungumza na mtu unapohisi huzuni, maumivu, uoga, hasira au aende na wewe kwa huduma ya matibabu na akusaidie kimawazo.

Chagua mtu anayekujali, mtu unayemwamini hatawaambia wengine, aliye na nguvu na wakujitegemea. Wakati mwingine mume wa mke aliyebakwa au wazazi huwa wamejawa na hasira kiasi cha kushindwa kupeana usaidizi.

Usijilaumu. Haukustahili kubakwa. Hukufanya kitu kilichompa mwanamume ruhusa ya kukubaka.


Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020313