Napaswa kujua nini kuhusu kondomu za wanaume
Kondomu ya wanaume ni mfuko mwembamba wa mpira ambao mwanaume huvaa kwenye uume wake kabla ya kushiriki ngono. Kwa sababu shahawa inakaa ndani ya mfuko, mbegu haziwezi kuingia katika mwili wa mwanamke.
Kondomu hutoa kinga kamili kutokana na mimba. Kinga hii huwa madhubuti ikiwa kondomu itatumika pamoja na dawa ya kuua mbegu na mafuta yanayotumika kurahisisha tendo la ngono.
Kondomu hazina madhara yoyote. Kondomu ni kinga bora dhidi ya magonjwa ya zinaa na virusi vya HIV. Kondomu zinaweza kutumika pekee au pamoja na njia nyingine ya kupanga uzazi. Kondomu zinaweza kununuliwa katika maduka ya madawa, na pia zinapatikana katika vituo vya afya na katika warsha za kuzuia UKIMWI.
Ni lazima kondomu ivaliwe wakati uume umesisimka, lakini kabla ya kugusa sehemu ya mwanamke ya siri. Ikiwa uume wake utagusa sehemu za mwanamke za siri au kuingia kwenye uuke, basi mwanamke atashika mimba au kuambukizwa magonjwa ya zinaa, hata kama hatamwaga shahawa (ejaculate).
Ikiwa kondomu itapasuka au kutoka kwenye uume, itabidi mwanamke aweke dawa ya kuua mbegu ndani ya uuke wake mara moja. Ikiwezekana, tumia mbinu ya mpango wa uzazi ya dharura.
Kumbuka: