Nawezaje kuepuka hatari za ubakaji
Tahadhari kwenda pahali popote ukiwa na mtu usiyemwamini au usiyemjua vyema.
Kuwa na namna ya kufika nyumbani ukiamua kuondoka. Ni kheri kutoenda pahali popote pale ikiwa huwezi kurejea nyumbani bila usaidizi wa mtu huyo.
Mweleze mtu huyo ya kwamba hupendezwi na matamshi yake au jinsi anavyokugusa. Asipobadilisha matendo yake, yafaa uondoke haraka iwezekanavyo.
Ikiwa mtu huyo yuko na mamlaka juu yako? (kwa mfano yeye ni mkubwa wako kazini, daktari wako, mwalimu, au mkubwa)
Mara ya kwanza afanyapo jambo ambalo halikupendezi, mweleze awache. Ikiwa anajaribu kutumia mamlaka yake, atatafuta mtu ambaye ni rahisi kumuogopesha. Mfahamishe ya kwamba huogopi.
Hatakufanyia mabaya (Kwa mfano kukufuta kazi, kukukataza huduma za afya, au kutokupa ruhusa) ikiwa utamkataza kukusumbua kabla hajafanya jambo litakalomfanya aonekane mjinga/mpumbavu.