Nawezaje kujilinda ikiwa niko tayari kwa tendo la ngono

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Nawezaje_kujilinda_ikiwa_niko_tayari_kwa_tendo_la_ngono

Unapoamua kuwa uko tayari kwa uhusiano wa kingono, lazima ujikinge kutokana na mimba na maambukizi. Kuna njia nyingi za kuhakikisha kuwa tendo la ngono ni salama. Hii inamaanisha kuwa unakuwa na mpango maalum kabla ya kushiriki ngono.

Zungumza na mpenzi wako kabla ya kushiriki ngono. Mueleze umuhimu wa kujikinga. Ikiwa unaona vigumu kuzungumza, labda fanya ionekane ni kama unazungumzia wapenzi wengine. Ikiwa anakujali, atataka sana kukulinda. Ikiwa anakushinikiza kushiriki ngono, labda anajijali tu.

Jamii nyingi zina watu ambao wamepata mafunzo ya jinsi ya kusambaza kondomu na mbinu zingine za kuoanga uzazi. Zungumza nao au muulize mhudumu wa afya pale unapoweza kupata mbinu ya kupanga uzazi. IKiwa unaona aibu, zungumza na mtu unayemuamini akusaidie. Baadhi ya kliniki za kupanga uzazi zian hudumu maalum kwa vijana na pia huwa na viajana waliopewa mafunzo ya kuzungumza na vijana wenzao na kuwapa mawaidha.

Kwa vile huwezi kutambua ikiwa mwanaume ameambukizwaugonjwa wa zinaa au virusi vya HIV kwa kumtazama tu, tendo la ngono ni salam tu ikiwa utatumia kondomu wakati wote. Ikiwa mwanaume ana kidonda kwenye uume wake au unatoa usaha, basi ana maambukizi na kwa hakika atakuambukiza!

IKiwa umeshiriki ngono na unatokwa na usaha kwenye sehemu yako ya uzazi, au una vidonda kwenye sehemu hiyo, au unahisi maumivu upande wa chini wa tumbo, huenda umeambukizwa ugonjwa wa zinaa.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020813