Nawezaje kutatua migogoro ya kazi za nyumbani

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Nawezaje_kutatua_migogoro_ya_kazi_za_nyumbani

Hizi hapa ni baadhi ya njia zitakazokusaidia kutatua migogoro ya kazi za nyumbani:

1. Usifikirie kuwa ni lazima utatue shida zako zote wewe mwenyewe. Usipowahusisha wengine kuhusu shida unazozipitia hutakuwa na msongamano wa mawazo pekee, bali yaweza kusababisha afya kudorora na kuadhiri familia yako pia. Kwa hivyo waelezee unaowaamini hisia zako. Hata kama shida zako hazitatatuliwa mara moja, kuwashirikisha wenzako kutapunguza mawazo na wasiwasi.

2. Jaribu kupata watu (familia, marafiki na majirani) wakusaidie na shida zako. Ikiwa hutapata usaidizi jaribu kuuliza tena ukitumia mbinu zingine tofauti kuelezea mambo yanayokusumbua. Kwa sababu sio kila mtu atakuelewa au kukusaidia, Mapema au baadaye mtu atatambua mahitaji yako na atakusaidia. Wakati mwingine wanaume hawatambui kwamba mwanamke anahitaji msaada kwa sababu wanafahamu kazi zote mwanamke anapaswa kufanya. Kwa hivyo jaribu kuishawishi familia yako kufanya kazi kama kikundi kimoja kwa niaba ya watoto wako.

3. Jaribu kumtia moyo mumeo atumie muda wake kwa kucheza na kuwatunza watoto wenu. Wanaume wengi hufikiria kwamba wanawake pekee ndiyo hupaswa kuwahudumia watoto wachanga, lakini hii si kweli, kwani takwimu zinaonyesha kuwa watoto wanaohudumiwa, na baba zao kimasomo na kutunzwa hukua vyema na walio na hekima wanapokuwa wakubwa, kwa hiyo muulize mumeo ikiwa anaweza kucheza, kuimba au kuzungumza na watoto wenu angalau mara moja kwa siku au muulize ikiwa anaweza kuwaosha na kuwabembeleza watoto walale.

4. Waeleze wanawake wengine shida zako. Wanawake huona haya kuzungumzia shida zao na wenzao kwa sababu hufikiria kuwa hakuna mtu atakayewaelewa au watu watawadharau ikiwa watazungumzia shida zao. Hata hivyo, kwa kutojitahidi kukutana au kuzungumza na wanawake wengine, wao hupoteza nafasi ya kupata, kupeana au kusaidia jamii. Mnaweza kutengeneza kikundi kidogo cha wanawake watakao kutana wakati fulani kuzungumzia shida zao kwa kuwaalika baadhi ya marafiki wako, marafiki zao, majirani au wanawake mnaofanya kazi nao mkutane pamoja. Utapata kwamba wengi wao wanapitia shida kama zako na wanaweza kutafuta njia za kusaidiana kwa mfano kwa kusaidiana kupika, kuwatunza watoto mara moja au mbili kwa wiki.

5. Fanya bidii upumzike muda baada ya muda hata kama shuguli za nyumbani hazijakamilika. Wanawake wengi huamini kwamba kushughulikia familia ni muhimu na hufikiri hawana haki ya kujitunza au kukimu mahitaji yao. Hii ni mbaya-ikiwa wanawake hawatakimu mahitaji yao watagonjeka na hatimaye familia zao zitalazimika kuwatunza. Kwa hivyo jaribu kuweka muda kila wakati kushughulikia afya na ustawi wako.


Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw021008