Nawezaje kuwakinga watoto wangu kutokana na kuzama

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Nawezaje_kuwakinga_watoto_wangu_kutokana_na_kuzama

Watoto wanaweza kuzama chini ya dakika mbili na katika kiasi kidogo cha maji hata kwa maji ya karai bafuni.

Kuzama majini kunaweza kusababisha bongo kuharibika au kifo. Ili kuzuia watoto wasizame, wazazi na wengine wanao walea watoto wanastahili kuwachunguza watoto walio karibu au ndani ya maji.

Palipo na maji, ni muhimu kufanya yafuatayo:

  • Funika visiwa/vidimbwi na mabomba ya maji ili watoto wasiweze kufungua.
  • Geuza karai iangalie chini wakati haitumiki na wachunguze watoto wanapooga.
  • Wafunze watoto kukaa mbali na mitaro na mifereji.
  • Kwa familia zinazokaa karibu na chemichemi ya maji, tengeneza ua itakayozingira nyumba, kisha funga mlango mkubwa kuwazuia watoto wachanga kuingia mle ndani ya maji.
  • Tengeneza ua la kuzingira mabwawa ya maji ukitumia reli zilizowima ziweke kwa matuta ya mchanga, madirisha na milango ili kuwazuia watoto kuzipitia.
  • Kwa familia zinzaoishi karibu na maji, weka mbao/ baa zikae wima kwa matuta ya mchanga, milango na madirisha ili kuzuia watoto kuanguka ndani ya maji.
  • Wafunze watoto jinsi ya kuogelea wangali wachanga.
  • Hakikisha umewavisha watoto wachanga ambao hawajui kuogelea life jacket wanapocheza kwa maji au ndani ya mashua.
  • Waelekeze na kuwachunguza watoto wanaoogelea.
  • Wafunze watoto kutokuogelea kwa mito iliyokasi na wasiwahi kuogelea pekee yao sehemu za mafuriko.
  • Waangalie watoto kwa umakini maji yanapopanda.
  • Hakikisha ya kwamba wahusika wote wa familia, hata watoto wakubwa wanaoelewa, wapate kujua sehemu salama wanazostahili kwenda ikiwa watahitaji kutoka nyumbani haraka.
Sources