Wafunze wanawe kuhusu uwezekano wa kuweza kuguswa katika hali ya kingono, na pia jinsi ya kutofautisha baina ya kuguswa kwa ishara ya mapenzi na kuguswa ambako hakuridhishi kwao.
Ikiwa itawezekana, watoto wa kike na wale wa kiume walale sehemu tofauti, haswa wakipitisha miaka kumi au kumi na moja.
Hakikisha watoto wako wanajua mtu ambaye wanaweza zungumza naye iwapo kuna jambo litatokea/kufanyika.
Muamini mwanawe anaposema hahisi vyema akiwa karibu na mtoto mwenzake au mtu mzima, bila kujali mtu huyo ni nani.
Wakati mwingine ukatili wa kijinsia kwa watoto huendelea kwa miaka mingi. Msichana anaweza kuambiwa kuwa ataumizwa au hata kuuliwa anapomwambia mtu anayoyapitia.
Sources
Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.