Nawezaje kuzuia kubakwa

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Nawezaje_kuzuia_kubakwa

Hakuna njia sawa au isio sawa ya kufuatwa ili kuepukana na kubakwa. Lakini kuna baadhi ya mambo mwanamke anafaa kufanya ili kupunguza uwezekano wa kubakwa.

Anachofanya mwanamke hutegemea anavyomjua mwanamume, anavyoogopa na kiwango cha hatari alichonacho. Kumbuka, mwanamke anapobakwa si eti alishindwa kuzuia ubakaji, lakini kwa sababu mtu aliyekuwa na nguvu kumliko alijilazimisha kwake.

Mambo yafuatayo yanaweza kumsaidia mwanamke yoyote yule kutobakwa:

  • Fanya kazi miongoni mwa wanawake wengine. Utakuwa salama na kupata nguvu zaidi ukifanya kazi katika vikundi.
  • Usimruhusu mtu yeyote anayekufanya uhisi wasiwasi nyumbani kwako. Usimjuze ya kwamba u pekee yako nyumbani.
  • Usitembee pekee yako, haswa nyakati za usiku. Inapobidi utembee pekee yako, tembea kwa ujasiri. Wabakaji wengi watamvamia mwanamke anayeonekana kuwa mnyonge wa kuvaamia.
  • Ukihisi kwamba unafuatwa, jaribu kubadiisha mkondo ufuate njia nyingine, unaweza hata kwenda kwa nyumba au duka la mtu mwingine. Pia unaweza geuka na kwa sauti ya juu umuulize anachotaka.
  • Beba chombo ambacho kitatoa sauti kubwa kama firimbi. Unashauriwa ubebe chombo unachoweza kutmia kujikinga. Yaweza kuwa kijiti, dawa ya kunyunyiza kwenye macho ya mbakaji wako, unga wa pilipili- ya kupuliza kwenye macho yake.
  • Ukivaamiwa, piga mayowe kwa sauti kubwa iwezekanavyo au tumia chombo ulichobeba cha kutoa sauti. Kama mambo haya hayatasaidia, jikinge kwa kumgonga upesi ili kumuumiza, ili uweze kupata nafasi ya kutoroka.
Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020307