Nawezaje kuzuia maradhi ya kuharisha

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Nawezaje_kuzuia_maradhi_ya_kuharisha

Watoto na pia watu wazima wanaweza kupata viini vinavyo sababisha kuharisha wakati wanapokula au kunywa maji yaliyo chafuka kwa kinyesi, au kwa kutumia viombo chafu au kwa kutozingatia usafi wa mahali pa kutayarishia chakula.

Ili kuzuia kusambaa kwa maradhi ya kipindupindu au kuharisha, inastahili:

  • Kuosha mikono kwa sabuni na maji safi au kwa njia zingine mbadala kama kwa kutumia jivu na maji safi; kila wakati baada ya kuenda chooni, baada ya kumbadilisha mtoto nepi, kabla na baada ya kutayarisha chakula, kabla kula au kuumpa mtoto chakula.
  • Kuzingatia usafi wa mazingara wanapochezea watoto. Ni muhimu pia kudumisha usafi nyumbani na kuwafunza watoto kunawa mikono vizuri na mara nyingi haswa baada ya kuenda choo na kabla ya kula.
  • Kuhakikisha kuwa kinyesi chote cha watoto au watu wazima kinatupwa kwenye choo au kimezikwa vizuri. Hakikisha pia uneosha maeneo yote yalioguzwa na kinyesi kwa kemikali za kuuwa viini.
  • Kutumia maji safi ya kunywa.
  • Kuosha vyema au kupika vizuri vyakula vyote: Bambua matunda na aina za mboga au uzisafishe kwa maji safi ikiwa watoto wanazila bila ya kupikwa. Tayarisha na upike chakula kwa umakini. Hakikisha chakula unachotayarisha kitaliwa chote. Hii ni kwa sababu masalio ya chakula yanaweza kuhifadhi viini vinavyo sababisha kuharisha. Masaa mawili baada ya chakula kuiva, hatari ya kuchafuka kwa viini visababishi kuharisha huongezeka ila kinapohifadhiwa kikiwa moto kabisa au baridi kabisa. Masalio yote ya chakula yanastahili kuzikwa, kuchomwa au kutupwa kwenye bomba la taka na kufunikwa ili kuwazuia inzi wanao weza kusambaza magonjwa.
  • Kumnyonyesha kwa kipekee, mtoto mchanga kutoka kuzaliwa hadi umri wa miezi sita na baadaye tena kwa miezi sita zaidi. Maziwa ya mama yana kiinga muhimu dhidi ya maradhi ya kuharisha.
  • Chanjo dhidi ya virusi vya rotavirus. Chanjo hii hupunguza vifo vinavyo sababishwa na virusi ya rotavirus.
  • Nyongeza ya vitamini A na madini ya zinki kwenye lishe. Vyakula vyenye vitamini A ni kama vile maziwa ya mama, ini, samaki, bidhaa za maziwa, matunda na aina za mboga zenye rangi ya njano au rangi ya machungwa na mboga za rangi ya kibichi. Madini ya zinki yanapo jumuishwa katika ratiba ya matibabu dhidi ya kuharisha, hupunguza makali na muda wa maradhi. Madini haya hupatiwa mtoto yakiwa tembe au dawa ya maji na humkinga mtoto dhidi ya kuharisha kwa muda wa hadi miezi miwili.


Sources