Nawezaje kuzuia ngono ya kulazimishwa

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Nawezaje_kuzuia_ngono_ya_kulazimishwa

Ikiwa anataka kushiriki ngono lakini wewe hutaki, unaweza kumwambia kuwa unafurahia kusifiwa lakini hauko tayari. Ikiwa unaogopa kuwa pamoja na huyu mtu, njoo na rafiki mwingine, au mwambie mtu mwingine azungumze naye.

Sema "LA" kwa sauti kubwa ikiwa unashinikizwa kushiriki ngono. Ikibidi, endelea kusema "LA". TUmia mwili wako pia kusema la. Ikiwa utasema "LA", lakini mwili wako unsema ndio, basi atafikiria kuwa unasema "ndio".

Songa mbali ikiwa utaguswa kwa njia ambayo haikupendezi. Hisia zako zinakutahadharisha kuwa kuna jambo lingine mbaya litatendeka. Piga kelele na uwe tayari kukimbia.

Usinywe pombe wala kutumia mihadarati. Pombe na mihadarati hupunguza uwezo wako wa kufanya uamuzi au kudhibiti yanayokutendekea.

Tembea kwa makundi. Katika maeneo mengi, wapenzi wengi huchumbiana wakiwa kikundi. Unaweza kuwa na mpenzi, lakini nivigumu ulazimishwe kushiriki ngono kwa sababu hamko peke yenyu.

Nenda sehemu ambapo wengine wanaweza kuwaona.

Fanya mipango yako mapema. Amua ni mguso upi zaidi ya ulivyotarajia. Usiache hisia zako zikuongoze na kufanya mambo yakutendekee.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020815