Nawezaje kuzungumuza na mume wangu au mpenzi wangu kuhusu upangaji uzazi
Ni sawa ukizungumza na mumeo au mpenziwe kuhusu mbinu za upangaji uzazi na mbinu mtakazo tumia.
Wanaume wengine hawataki bibi zao kutumia mbinu za upangaji uzazi, kwa sababu hawajui sana jinsi mbinu hizo tofauti zinazofanya kazi. Mwanamume anaweza kujali afya ya mkewe kwa sababu amesikia hadithi tofauti tofauti kuhusu hatari za upangaji uzazi. Wanaume wengi huogopa kwamba wanawake wao watakuwa na uhusianao wa mapenzi na wanaume wengine wakitumia mbinu hizi za upangaji uzazi au hudhania kuwa na watoto wengi nikuonyesha uume.
Jaribu kusambaza mawaidha haya yaliyoko kwa ukurasa huu. Yaweza kuelimisha mume wako kuelewa kwamba:-
Ikiwa mumeo hataki utumie njia za upangaji uzazi hata baada ya kujifunza umuhimu wa upangaji uzazi, unastahili ufanye maamuzi ikiwa utatumia mbinu za upangaji uzazi. Ikiwa utafanya uamuzi, unastahili uchague mbinu itakayotumika bila mumeo kujua.