Nawezaje zuia watoto wangu kutokana na majeraha ya kuungua na moto au miale ya moto

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Nawezaje_zuia_watoto_wangu_kutokana_na_majeraha_ya_kuungua_na_moto_au_miale_ya_moto

Ili kuzuia aina hii ya jeraha:

Weka watoto wachanga mbali na moto wa kupika, vibiriti, taa ya mafuta, mishumaa na miminiko yanayoweza kushika moto kama vile mafuta ya taa

Weka jiko katika eneo lililo sawazishwa na juu pale watoto hawawezi kufikia.

Kama moto ulio wazi utatumika, tengeneza katika kifusi cha udongo kilicho inuliwa, si kwa ardhi moja kwa moja. Kizuizi cha udongo, mianzi au vifaa vingine vyovyote vile, au playpen yaweza tumika kuzuia watoto wachanga kufikia eneo la kupikia.

Usiwache watoto wachanga pekee yao karibu na moto au kuwa na moto au kupika.

Weka watoto mbali na chuma ya kuchemsha maji au kwa kimombo (heaters) pasi moto na vifaa vingine moto

Usiwahi kumwacha mtoto pekee yake katika chumba na mshumaa unawaka au moto unawaka.

Sources