Ni aina zipi za upangaji uzazi bado zipo

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Ni_aina_zipi_za_upangaji_uzazi_bado_zipo

Mara tu unapoamua kutumia upangaji uzazi, lazima uchague mbinu. Ili kufanya uamuzi bora ni lazima ujifunze kwanza kuhusu mbinu tofauti, faida na hasara zake.

Kuna aina 5 kuu za upangaji uzazi:

  • Mbinu za kuzuia, ambazo huzuia mimba kuingia kwa kuzuia shahawa kufikia yai.
  • Mbinu za Homoni, ambazo huzuia ovari ya mwanamke kutoa yai, huwa vigumu kwa shahawa za kiume kufikia yai, na huzuilia nyumba ya uzazi kubeba mimba.
  • IUDs, ambazo huzuia shahawa ya mwanamume kuchanganyikana na yai la mwanamke.
  • Mbinu asili, ambazo husaidia mwanamke kujua wakati yuko tayari kushika mimba, ndiposa aweze kuepuka kufanya ngono wakati huo.
  • Mbinu za kudumu. Hii ni oparesheni inayofanywa kwa mwanamke au mwanamume na humfanya kukosa watoto kabisa baada ya oparesheni hiyo.
Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020407