Ni aina zipi za upangaji uzazi zinanifaa kutumia baada ya kuavyaa mimba

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Ni_aina_zipi_za_upangaji_uzazi_zinanifaa_kutumia_baada_ya_kuavyaa_mimba

Baada ya kuavyaa mimba unaweza kupata mimba tena mara moja-kwa haraka kama wiki mbili. Mbinu nyingi za upangaji uzazi huchukuwa muda ndio zifanye kazi, kwa hivyo ongea na mtu kuhusu upangaji uzazi na uanze kutumia moja ya mbinu hizi mara moja iwezekanavyo.

Kidonge: waweza kuanza kumeza vidonge siku io hiyo ya utoaji mimba. Usingoje zaidi ya wiki moja.

Kifaa kiingizwacho ndani ya mfuko wa uzazi (IUD): Kama hakuna hatari ya maambukizi, mtaalamu wa afya anaweza kuweka ndani kifaa cha mfuko wa uzazi (IUD) mara tu baada ya kuavyaa mimba.

Sindano: Sindano ya kwanza yafaa kupewa siku ya kuavyaa mimba, au hadi wiki moja baadaye.

Implants: Implants yaweza kuwekwa kabla tu au baada tu ya utoaji mimba, au hadi wiki moja baadaye.

Matibabu ya kike ya kufanya mwanamke asizae tena. :

Kama mimba yako ilikuwa chini ya miezi mitatu, waweza kuchanjwa ili usizae tena wakati wa kuavyaa mimba au mara tu baada yake. Ni muhimu zaidi wewe kufanya uamuzi huu kwa makini. Chanjo ya kufanya mwanamke asizae tena ni ya kudumu.

Matibabu ya kufanya wanaume kutoweza kufanya mwanamke kupata mimba:

Matibabu hayo kwa mwanaume yawezafanywa wakati wowote na ni ya kudumu. Uamuzi lazima ufanywe kwa makini.

Kondomu au mpira: wewe na mpenzi wako mnaweza kutumia kondomu mnaposhiriki ngono tena. Kondomu huzuia dhidi ya magonjwa ya zinaa(STIs), ikiwa ni pamoja na VVU (Virusi Vya UKIMWI)

Spermicide: waweza tumia spermicide mara tu unaposhiriki ngono tena. usitumie spermicide kama uko na Virusi Vya UKIMWI, au kama uko na wapenzi wengi.

Kiwambo: Kama hakuna maambukizi au jeraha, waweza fungwa na kiwambo baada ya utoaji mimba.

Njia za kiasili (kamasi na kuhesabu masiku): Njia hizi hazifanyi kazi hadi hedhi yako ya kawaida kurejea.



Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020210