Ni chanjo zipi anazostahili mtoto wangu

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Ni_chanjo_zipi_anazostahili_mtoto_wangu

Watoto wote wanastahili kupokea chanjo itwayo BCG (Bacile Calmette-Guérin) vaccine. Hii huumpa mtoto kinga dhidi ya aina zingine za kifua kikuu na ukoma. Hata hivyo, kinga hii si kamili.

Watoto wote wanastahili chanjo dhidi ya dondakoo, pepopunda na kifaduro kupitia aina ya chanjo iitwayo DTP au DPT vaccine. Viini vya dondakoo husababisha maambukizi ya njia ya kuingizia hewa na huenda ikasababisha shida za kupumua na hata kifo. Pepopunda nayo husababisha kukauka kwa misuli na maumivu makali yanayo sababishwa na mkazo wa misuli. Mkazo huo wa misuli unaweza sababisha kifo. Kifaduro huathiri njia ya kuigizia hewa na kusababisha kikohozi kinachoweza dumu wiki nne hadi nane na ni hatari sana kwa watoto wachanga.

Wanawake wote waja wazito na watoto wachanga wanahitaji chanjo ya pepopunda.

Watoto wote wanastahili kupokea chanjo dhidi ya surua. Maradhi ya surua husababisha utapiamlo, udhaifu wa maendeleo ya ubongo na huweza kufanya mtoto kiziwi au kipofu. Ishara zinazoelekeza kuwa mtoto anaweza kuwa anaugua surua ni pamoja na kuongezeka kwa joto mwilini, upele, kikohozi, kumwaga kamasi na macho kubadilika na kuwa mekundu. Tahadhari, mtoto anaweza kufa kutokana na surua.

Watoto wote wanastahili chanjo dhidi ya polio. Dalili za polio ni utepe kwenye mguu au mkono na udhaifu wa kukitumia kiungo kilicho athirika. Kwa kila watoto mia mbili wanaoambukizwa maradhi ya polio, mmoja atapata ulemavu wa maisha.

Ratiba za chanjo hutofautiana kulingana na nchi au sehemu ya nchi unayoishi. Ni muhimu kufuatilia ratiba ya chanjo kwa mujibu wa mwongozo wa taifa. Watoto wanastahili kupokea chanjo kwa umri unaostahili na kwa muda unaostahili.

Sources