Ni mbinu zipi za kuavyaa mimba zilizo salama

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Ni_mbinu_zipi_za_kuavyaa_mimba_zilizo_salama

Mimba yaweza kutolewa kutoka kwa tumbo la uzazi na mhudumu wa afya aliye na ujuzi katika njia zifuatazo.

Kuavya mimba kwa njia ya kufyonza

Mimba hutolewa kwa kutumia mrija maalum (Cannula) ambao huwekwa tumboni kupitia uke wa mwanamke na mfuko wa uzazi. Hii inaweza kufanywa bila ya kumpa dawa za kulala mwanamke ingawaje wakati mwingine dawa hudungwa kwenye mfuko wa uzazi kupunguza uchungu. Wakati utaratibu huu unapofanywa kwa mkono, mimba hutolewa kutumia sindano maalum. La sivyo utaratibu huo hufanywa na mashini ya kielektroniki. MVA ni rahisi na salama huchukua takriban dakika 5 au 10 tu. Utaratibu huu hufanywa katika zahanati au kituo cha afya au afisi ya daktari. Aina hii ya uavyaji mimba ni salama kufanya katika kipindi cha wiki 12 au miezi mitatu ya mimba.

Kutolewa kwa mimba kwa kugema (Kupanuliwa na kifaa, au D na C)

Mimba hugemwa na kifaa kiitwacho curette, kifaa kinachofanana na kijiko kilichotengenezwa kuingizwa ndani ya tumbo la uzazi. Kifaa hicho kiitwacho curette ni kikubwa kuliko kifaa kiitwacho cannula na sababu ni kimenolewa, mfuko wa uzazi lazima ufunguke. Kupanuka huko kunaweza kusababisha uchungu. Aina hiyo ya D na C huchukua muda kiasi (kama dakika 15 hadi 20) huwa ni chungu zaidi na ghali. Huwa hufanywa katika chumba cha oparesheni, na mwanamke hupewa dawa ya kumfanya alale.

Kuavyaa mimba kwa kutumia dawa

Dawa zingine za kisasa hutumika na madaktari na wahudumu wa afya ulimwenguni kusababisha utoaji wa mimba. Hii huitwa utoaji wa mimba kwa kutumia dawa. Dawa hizi hufanya tumbo la uzazi kupanuka na kusukuma ile mimba. Dawa hizi humezwa au kufuta mdomoni. Wakati dawa hizi zinapotumika vyema, basi utoaji mimba hufanyika vyema na salama. Kwa sababu hakuna kitu kiwekwacho kwa tumbo la uzazi, hatari ya kuambukizwa maradahi haipo ambayo huuwa wanawake wengi ambao huavyaa mimba vibaya.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020208