Ni vipi naweza kuikinga familia yangu ikiwa ugonjwa utakurupuka

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Ni_vipi_naweza_kuikinga_familia_yangu_ikiwa_ugonjwa_utakurupuka

Kwa dharura, ukosefu wa maji safi na usafi waweza kusababisha ugonjwa utakao kuwa janga kubwa. Kipindupindu hutokea mahali ambapo usafi ni duni na kunapo msongamano wa watu.

Janga au kukurupuka kwa maradhi hayo kunaweza sababisha dharura kwa sababu ya ukali wa ugonjwa huo. Kwa kisa cha homa ya mafua na magonjwa mengine yanayosambazwa kwa watu kugusana, walio wagonjwa wanapaswa kuwekwa kando.

Dalili ya mafua ni pamoja na joto nyingi, kikohozi, kuumwa na koo au vidonda vya koo, maumivu ya mwili, kuumwa na kichwa, baridi, uchovu, kutapika na kuhara. Katika baadhi ya matukio, mafua yaweza kusababisha pneumonia na matatizo ya kupumua.

Njia rahisi za kufuata ni:-

  • Nawa mikono mara kadhaa ukitumia sabuni na maji au jivu na maji
  • Zika takataka na kinyesi salama.
  • Jifunze njia salama za maandalizi ya chakula
  • Tumia njia salama za kupata maji safi au chemsha maji, chuja maji, ongeza chlorine au weka maji kwa jua.
  • Hifadhi maji ha kunywa kwa mikebe iliyo safi.
  • Kaa nyumbani ikiwa wewe ni mgonjwa mbali na wenzako.
  • Pata kujua dalili na ishara hatari, na wapi pa kuenda au kupata msaada ikiwa ugonjwa utaendelea.
  • Kila mahali pawe safi.
  • Funika mdomo kwa kutumia kitambaa au karatasi ya sashi ukikohoa na uzike vyema karatasi hiyo.
  • Usiteme mate hadharani au karibu na watoto
  • Kaa angalau mita moja mbali na wenzako haswa ikiwa wanakohoa, kupiga chafya au kuonekana wagonjwa.
  • Kaa nyumbani na usijumuike na mikutano ya hadhara na kusafiri.
Sources