Ni vipi naweza kumzuia mtoto wangu kunyongwa

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Ni_vipi_naweza_kumzuia_mtoto_wangu_kunyongwa

Njia moja ambayo watoto huchunguza mazingira ni kwa kuweka vitu kwa midomo ambavyo vinaweza kuwanyonga.

Watoto wadogo, pia huwa na wakati mgumu wa kutafuna na kumeza vyakula vingine kama peremende ngumu ambazo huwanyonga.

Wazazi au walezi wanapaswa kufanya hivi:

Hakikisha mahali pa kucheza na kulala ni salama, pasiwepo na vitu vidogo kama vifunguo, shanga, vibofu, makopo ya kalamu, sarafu, tembe na karanga.

  • Angalia vizuri vitu vya kuchezea vya watoto vipya kabla watoto hawajaanza kuvitumia ili kuhakikisha havilegei au kuwa na vitu vilivyonolewa ambavyo vinaweza kumezwa au kuhatarisha usalama wa mtoto.
  • Usiwahi kumpa mtoto mdogo vyakula ambavyo vimaweza kumnyonga kama Njugu (karanga), peremende ngumu au mifupa midogo au mbegu.
  • Hakikisha unawaelekeza watoto wadogo wakati wa kukula kisha katakata au gawanya chakula cha watoto katika vipande vidogo vidogo ambavyo vinaweza kutafunwa au kumezwa kwa urahisi.

Kukohoa, Kushindwa kuongea, kupumua kusiko kwa kawaida au kushindwa kutoa sauti kabisa kunaonyesha usumbufu wamkupumua na kusababisha kunyongwa.

  • Wazazi na walezi wanastahili kushuku kuwa mtoto amenyongwa wakati anapoanza kwa ghafla kupumua au kuhema kwa shida hata kama hakuna mtu aliyemuona mtoto huyo akiweka kitu mdomoni.


Sources