Ni vipi nitakavyokabiliana na migogoro ya matibabu na elimu ya wasichana wangu

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Ni_vipi_nitakavyokabiliana_na_migogoro_ya_matibabu_na_elimu_ya_wasichana_wangu

Unaweza kutumia mawazo haya kumshawishi mume wako awape wasichana wako elimu bora:

Ni mawazo na matendo bora ya wazazi ya kuwalea na kuwakubali watoto wao wote kwa njia iliyo sawa ambayo inaweza na lazima ibadilishe jamii nzima, haijalishi ikiwa ni wa kiume au wa kike. Mtoto wa kike anastahili kupewa nafasi kwa kila hali sawa na vile wa kiume hupewa sababu watoto wa kike ni wa thamani kama wa kiume.

Wasichana si eti hawana uwezo wa kuwashinda wavulana kwa kila namna. Kinyume na hayo, katika shule na chuo kikuu, wasichana huwa wanawashinda wavulana. Ikiwa ushahidi utahitajika, mueleze matokeo ya hivi karibuni ya mtihani wowote ule.

Watu hutaka wakwe waliosoma lakini husita kuwaelimisha wasichana wao. Hii si sawa wala haileti picha.

Kuna msemo unaojulikana sana unaosema: "Ukimuelimisha msichana wako, umeelimisha familia mbili. " Hii inahusiana vyema na majadiliano haya kwa sababu, ukimuelimisha kijana umemuelimisha mtu mmoja pekee ilihali ukimuelimsha msichana haumuelimishi yeye pekee yake bali familia mpya baadaye.

Elimu imehusishwa kwa karibu na ajira. Elimu mbaya inamaanisha hadhi ya chini na malipo duni ya ajira. Elimu ni hatua muhimu sana mzazi anaweza kufanya kwa kujaribu kupandisha hadhi ya msichana wake na kumfanya aweze kujitegemea kifedha.



Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw021012