Ni vipi niwezavyo kuavyaa mimba salama

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Ni_vipi_niwezavyo_kuavyaa_mimba_salama

Si rahisi kujua kama uavyaji mimba utakuwa salama. Jaribu kuenda pale ambapo utaavya mimba ua uliza yule ambaye ameshawahi kuwa hapo maswali haya.

  • Umewahisikia wanawake wanagonjeka au kufa kutokana na kutoa mimba mahali hapa? Kama ni kweli, nenda pahali pengine
  • Nani atakaye nihudumia na walifunzwaje? Madaktari, wauguzi, wafanyikazi wa afya na wazalishaji wa kimila wanaweza. Hata hivyo, utoaji mimba unaofanywa na asiyefunzwa mbinu za usalama za kutoa mimba na njia ya kukinga maradhi unaweza kuwa hatari sana.
  • Chumba cha kutoa mimba ni safi na umepangwa vilivyo? Kama ni chafu na umeharibika, labda pia utoaji mimba utakuwa hivyo.
  • Kuna mahali pa kunawa mikono? Mhudumu wa afya ambaye hana mahali pa kunawa mikono yake hawezi kufanya utoaji mimba safi na wa usalama.
  • Je, vyombo vinakaa kama vinapatikana au vimetengenezwa nyumbani? Vyombo vinavyotengenezwa nyumbani huweza kusababisha majeraha au maradhi.
  • Ni vipi vyombo hivyo vinasafishwa au kufanywa visiwe na viini vya uchafu? Vyombo vinafaa vitumbukizwe kwa maji yaliyo na dawa au maji yaliyochemshwa kuuwa viini vya uchafu vinavyosababisha maradhi.
  • Bei ni nafuu? Kama bei ni ya juu sana, mara nyingi inamaanisha mhudumu wa afya anajali tu pesa na si afya yako.
  • Kuna huduma zingine za kiafya zinazopewa pamoja na kutoa mimba? Kituo cha huduma cha afya nzuri pia kitajaribu kupeana huduma zingine ambazo wanawake wanahitaji, kama upangaji uzazi, tiba kwa maradhi ya ngono, na jinsi ya kuepukana na virusi vya ukimwi
  • Ni wapi utapelekwa ikiwa jambo lisilostahili kufanyika wakati au baada ya kutoa mimba?
  • Lazima kuwe na mpango wa kukupeleka hospitalini kama kuna kisa cha dharura.

MUHIMU: Uavyaji mimba ni hatari zaidi kama:

  • Kutoka kwa damu kwako ulikuwa zaidi ya miezi tatu baadaye.
  • Mimba yako imeanza kuonekana.

Wakati unapokaa na mimba kwa muda zaidi, ndipo fursa zaidi za matatizo baada ya kutoa mimba. Kwa usalama wako, kuavyaa mimba baada ya miezi mitatu lazima kufanywe na vifaa maalum katika zahanati au hospitali.


Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020209