Nifanye maamuzi yapi kuhusu kuavyaa mimba

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Nifanye_maamuzi_yapi_kuhusu_kuavyaa_mimba

Uamuzi wako wa kuavyaa mimba utategemea ikiwa kuna njia salama za kuavya amimba unakoishi. Inategemea pia jinsi uavyaji wa mimba au mtoto utaadhiri maisha yako.

Inaweza saidia ukitafakari haya maswali:

Je utaweza kumtunza mtoto? Je una pesa za kutosha za kumlea mtoto?

Je ujauzito ni tisho kwa afya yako?

Unaye mpenzi au mume atakaye kusaidia kumlea mtoto? Unaweza kuzungumza naye kuhusu uamuzi huu?

Dini au familia yako inakashifu uavyaji wa mimba? Kama ndio, utahisi vipi ukiavyaa mimba?

Uavyaji wa mimba utafanywa vipi?

Umekuwa mja mzito kwa muda gani?

Je unaweza kuwa na ugonjwa wa zinaa au virusi vya ukimwi? Unaweza kuwa katika hatari ya kupata magonjwa ya zinaa kama wewe ni mchanga, hujaolewa, na una mpenzi mpya, au kama una dalili za ugonjwa wa zinaa. ukihisi ikiwa na hatari, unaweza kuhitaji matibabu kabla ya kuavyaa mimba.

Ni matatizo gani yanayoweza kusababishwa na uavyaji wa mimba? Kama una virusi vya ukimwi, hatari za kuavyaa mimba kwa hatua zisizo salama huongezeka.

Utaenda wapi kupata usaidizi wa dharura ukipata matatizo? Utafika huko vipi?

Ikiwa uavyaji wa mimba wa njia salama haupatikani, unaweza fikiria kumpeana yule mtoto, hii ni kama inakubalika na jamaa yako na wewe mwenyewe pia.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020207