Nifanye nini ikiwa namjua aliyebakwa

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Nifanye_nini_ikiwa_namjua_aliyebakwa

Mhakikishie ya kwamba si makosa yake. Msaidie. Sikiliza hisia zake, msaidie kuamua anachotaka na umuhakikishie ya kwamba anaweza kuendelea na maisha.

Heshimu anachokitaka kwa ajili ya usalama wake wa kibinafsi. Usimwambie mtu mwingine yule bila idhini yake.

Mpeleke kuona mhudumu wa afya, kuripoti ubakaji huo kwa polisi, kuzungumza na mtu aliyefundishwa kumsikiza na kumsaidia, kumuona wakili, na kwenda kortini ikiwa atataka kufanya hivyo.

Msimlinde mbakaji ikiwa mnamjua. Ni hatari kwa usalama wa wanawake katika jamii.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020314