Nifanye nini ikiwa ninamjua mtu anayetaka kujiua

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Nifanye_nini_ikiwa_ninamjua_mtu_anayetaka_kujiua

Daima kuwa maakini na matamshi ya kujiua. Wakati mtu atakaposema anafikiria kujiua, jua kuwa hiyo ni ishara wazi ya kujiua. Tafuta msaada kutoka kwa mtaalamu haraka iwezekanavyo.

Ikiwa mtu atakuambia ya kwamba unastahili kuweka siri nia yake ya kujiua, usikubali. Katika hali yoyote ile hustahili kuweka siri hiyo inayoweza kusababisha kifo cha mtu huyo. Utakuwa umesaidia kifo chake ikiwa utaweka siri, jambo ambalo linaloweza kukusumbua maishani mwako. Badala yake chukua hatua zitakazozuia mtu kujiua.

  • Usishtuke. Anayetaka kujiua yuko na mawazo mengi na ikiwa utashtuliwa na kinachosemwa, anayetaka kujiua atakuwa na msongamano wa mawazo zaidi. Tulia.
  • Sikiliza kwa umaakini anachotaka kusema mtu huyo. Mruhusu aongee. Sikiliza kwa karibu ndiposa uweze kumsaidia iwezekanavyo na ujue kinachosabisha hisia zake za kujiua.
  • Mfariji mtu huyo na maneno ya faraja. Tumia akili uliyonayo kumshauri. Kuwa mpole na anayejali kwa vyovyote iwezekanavyo.
  • Acha mtu atambue ya kwamba unamjali. Mwambie na uonyeshe ya kwamba unamjali.
  • Usimhukumu kwa matendo yake. Usibatilishe anachosema au kuhisi. Msaidie na umjali, sio kumhukumu, lakini tafuta usaidizi haraka iwezekanavyo. Msaada waweza kutoka kwa wahusika wa familia yake au marafiki, mradi wasisababishe kujinyonga kwa jamaa wao, au mfanyakazi wa dharura au mtaalamu anaweza kuwa wa maana kwa kutoa usaidizi.
  • Ikiwa mtu huyo yuko katika hatari kubwa ya kujiua, usimuache pekee yake, hata kwa sekunde chache.
  • Baada ya mtu huyo kupata usaidizi na hayuko katika hatari kubwa ya kujiua, msaidie kuchagua siku ya kumuona mhudumu wa afya au mtaalamu husika. Hisia za kujiua zinahitaji zishughulikiwe na wataalamu pekee. Wataalamu husika wanastahili kuendelea kumshauri na kumtunza mtu huyo.


Sources
  • Felicitas Heyne, Psychologist
  • Audiopedia ID: sw020916