Nifanye nini kutokana na mikwaruzo ya uke baada ya kubakwa

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Nifanye_nini_kutokana_na_mikwaruzo_ya_uke_baada_ya_kubakwa

Wakati mwingine ubakaji huharibu sehemu za siri. Hii husababisha uchungu, lakini uchungu huo hupotea baada ya muda. Ikiwa unatoa damu sana, utahitajika kumuona mhudumu wa afya aliye na ujuzi wa kushona sehemu yako ya siri iliyoharibika.

Ikiwa umeumizwa kidogo:-

  • Lowesha sehemu yako ya siri mara tatu kila siku ndani ya maji vuguvugu ambayo yamechemshwa kisha yakapoeshwa. Weka majani ya chamimile ndani ya maji yanayochemka kwani yatasaidia kupoesha uchungu na mikwaruzo uliyoipata. Au unaweza kuweka gel itokayo kwa mti wa aloe katika mikwaruzo uliyonayo.
  • Mwaga maji katika sehemu yako ya siri unapokojoa ndiyo usichomeke. Kunywa vitu vilivyo na maji maji mengi hufanya mkojo kuwa bila nguvu kwa hivyo hutachomeka sana.
  • Chunguza au angalia dalili/ishara za maambukizi: joto, usaha wa rangi ya manjano, harufu mbaya, na uchungu unaozidi.
  • Baada ya kubakwa, ni kawaida kwa wanawake kupata maambukizi ya kibofu cha mkojo au maambukizi ya figo.


Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020319