Nifanye nini kwa ajili ya usalama wangu kabla ya vurugu kutendeka tena

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Nifanye_nini_kwa_ajili_ya_usalama_wangu_kabla_ya_vurugu_kutendeka_tena

Mwambie mtu wa karibu kuhusu vurugu. Muulize mtu huyo aje au atafute msaada ikiwa atasikia kuwa uko taabani. Labda jirani, ndugu wa kiume, au kikundi cha wanawake au wanaume wanaoweza kuja kabla ya wewe kuumizwa.

Tafuta mtu unayemwamini ambaye anaweza kukusaidia kutatua hisia zako na anayejali maamuzi yako.

Fikiria neno maalum au ishara utakayo tumia kuwaambia watoto wako au mtu mwingine katika familia yako kutafuta msaada.

Wafunze watoto wako jinsi ya kufikia mahala salama.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020116