Nifanye nini nikishambuliwa kimapenzi

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Nifanye_nini_nikishambuliwa_kimapenzi

Ikiwa mwanamke atafaulu kumshinda mmbakaji, basi atafaulu kujikinga kubakwa hata kama mmbakaji yuko na silaha. Njia nyingi atakazozitumia mwanamke kujikinga kubakwa, ndizo zitakazomsaidia kuepuka kubakwa au kupata majeraha kiasi na matatizo ya kiakili kutokana na ubakaji baadaye.

Ni vigumu kujua mapema jinsi mwanamke atakavyofanya anapotaka kubakwa. Wanawake wengine hupandwa na hasira na kupata nguvu wasiojuwa walikuwa nayo. Wengine hushindwa kutembea. Ikiwa utajipata katika tukio hili, jua utakaloweza kufanya.

Mambo haya yataweza kukusaidia wakati wa ubakaji:-

  • Usilie, kumsihi, au kukubali. Hii haisaidii. Mwanzo wanawake wanaojaribu jambo hilo huumia sana kuliko wanawake wanaojitetea.
  • Kaa chonjo. Mwangalie mbakaji vyema. Huenda kukawa na wakati asiyokuangalia au hata kushindwa.
  • Jaribu njia tofauti. Mpige mateke, piga nduru, jadilianeni, muekee mtego--fanya lolote litakalomfanya aone kuwa wewe sio muathiriwa rahisi. Mfanye aelewe ya kwamba wewe ni binadamu sio kifaa.
  • Ikiwa unamjua mbakaji, mueleze jinsi unavyohisi. Usimfanye afikirie ya kwamba wanawake hufurahia kubakwa. Mfahamishe anachokifanya.
  • Ikiwa humjui mbakaji, jaribu kutambua sura yake. Ni mkubwa kivipi? Yuko na alama yoyote, au mchoro mwilini? Amevaa nguo zipi? Jaribu kukumbuka ndiposa uelezee polisi na kuwaonya wanawake wengine katika jamii yako.
  • Ikiwa kunao watu wengi wanaotaka kukubaka, au ikiwa mbakaji yuko na silaha, bado unaweza kukataa lakini si vyema kupigana na mbakaji.
  • Fikiria vyema. Ndiposa unaweza kuamuwa ikiwa unastahili kupigana naye. Katika visa vingine vya ubakaji, kwa mfano, wakati wa vita, mbakaji anaweza kosa sababu ya kukuwacha hai ikiwa utakataa.


Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020312