Nifanyeje ikiwa nitahisi kujiua

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Nifanyeje_ikiwa_nitahisi_kujiua

Ikiwa umekuwa ukihisi unyogovu kwa muda mrefu;kuhisi kama hauna matumaini, hauna njia ya kukabiliana na matatizo yote unayokumbana nayo kila siku, na huoni chochote cha thamani maishani, basi unaweza kufikiria, kujiua ni suluhisho la pekee. Hata hivyo, ukweli ni kwamba kujiua ni tatizo, sio suluhisho. Hata kama unafikiria ya kwamba hakuna suluhisho la matatizo yako sasa hivi, haimaanishi suluhu lingine halipo na halitapatikana siku za usoni. Inamaanisha ya kwamba huwezi kuona suluhisho hilo kwa wakati huo na unastahili ushikilie kwa nguvu hatamu za maisha.

Fikiria kwa dakika: Je, unahisi kufanya hivyo sasa hivi? nafasi ni; kuna nyakati katika maisha yako wakati hukujali sana, wakati ambapo mambo hayakuwa mabaya, labda hata mambo yalikuwa mazuri. Kwani hiyo haimaanishi kuwa mambo fulani katika maisha yako yalibadilika kukufanya uhisi mnyonge?Na kama yalikuwa ni mabadiliko yaliyosababisha uchungu mwingi kwani haimainishi kuwa mabadiliko mengine yanaweza kuondoa uchungu? Kwa hivyo kuwa na subira, siku itafika ambapo mambo yatabadilika kuwa mazuri. Maisha ni mzunguko wa furaha na huzuni.

MAMBO MUHIMU YA KUTAMBUA:

  • Usijilaumu kwa hisia za kujiua. Mahangaiko ya maisha ni sehemu tu ya maisha. Si kosa lako.
  • Kutaka kujiua hakukufanyi wewe kuwa mtu mbaya, au mwendawazimu, mnyonge au mjanja.
  • Haimaanishi kiukweli unataka kufa - yamaanisha ya kwamba uko na machungu ambayo yanakushinda kuyakabili kwa sasa. Ikiwa mtu atakuwekelea uzito juu ya mabega yako, hatimaye utaanguka ikiwa ataendelea kuongeza uzito, haijalishi kiasi gani unataka kusimama bado. Hii ni kawaida.

Mawazo haya yanaweza kukusaidia uyashinde mawazo yako ya kujiua:

  • Zungumza na mtu atakaye kusaidia(iwe rafiki, mpenzi, jamaa, mtu anayejulikana au mgeni atakaye kusaidia)
  • Muone daktari, mtaalamu au mfanyakazi wa afya.
  • Fikiria maumivu ya wale utakao waacha nyuma.
  • Usitumie majaribio ya kujiua kama njia ya kulipiza kisasi, au kutuma ujumbe '
  • Tafuta msaada wa wengine wanaopitia hali kama hiyo, kama kikundi cha msaada au kitu sawa na hicho.
  • Usifanye jambo kutokana na msukumo.
Sources
  • Felicitas Heyne, Psychologist
  • Audiopedia ID: sw020909