Nifanyeje nikikosa kumeza kidonge

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Nifanyeje_nikikosa_kumeza_kidonge

Ikiwa utakosa kumeza kidonge/dawa unaweza kupata mimba. 

Ikiwa utasahau kidonge kimoja au viwili, meza dawa moja maramoja utakapokumbuka. Kisha meza kidonge kifuatacho kwa muda wa kawaida. Hii inaweza kumaanisha kuwa umeze vidonge viwili kwa siku moja.

Ikiwa utasahau kumeza kidonge cha tatu, siku tatu mfululizo, meza kidonge kimoja mara moja. Kisha meza kidonge kimoja kila siku kwa muda wa kawaida.

Ikiwa unatumia pakiti ya dawa ya siku 28, meza vidonge vya homoni pekee na uruke vidonge vya sukari, kisha anza kumeza vidonge vya homoni kutoka kwa pakiti moja. Ikiwa unatumia pakiti ya siku 21, anza kutumia pakiti mpya haraka iwezekanavyo ukimaliza kutumia unayotumia sasa hivi. Tumia kondomu (au usishiriki ngono) hadi utakapomaliza kidonge kwa siku saba mtawalia/mfululizo.

Ikiwa utasahau kuchukua zaidi ya vidonge vitatu, acha kutumia vidonge na usubiri siku zako za hedhi/mwezi. Tumia kondomu/mpira ( au usishiriki ngono) katika siku zako za hedhi. Kisha anza kutumia pakiti mpya.

Kuchelewa au kukosa kutumia vidonge, kunaweza kusababisha kutokwa na damu, kama damu kidogo ya siku za hedhi.

Ikiwa uko na matatizo ya kukumbuka kumeza vidonge, jaribu kumeza kidonge wakati wa kufanya kazi za kila siku, kama kuandaa mlo wa jioni. Au meza kidonge wakati jua linapotwaa/ magharibi au kabla ya kulala. Weka pakiti mahali ambapo unaweza kuiona kila siku. Ikiwa bado utasahau kumeza kidonge/dawa mara kadhaa (zaidi ya mara moja kwa mwezi), fikiria kubadilisha na kutumia mbinu nyingine ya upangaji uzazi.

Ikiwa utatapika kati ya masaa matatu baada kumeza kidonge au kuharisha, Kidonge chako cha upangaji uzazi hakitakaa katika mwili wako muda wa kutosha kufanya kazi vyema. Tumia kondomu, au usishiriki ngono, hadi pale utakapohisi vizuri na utakapo kunywa kidonge kila siku kwa siku saba.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020427