Nijitayarishe kwa mambo gani ikiwa nitaondoka

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Nijitayarishe_kwa_mambo_gani_ikiwa_nitaondoka

Ikiwa utaamua kuondoka, utahitajika kujiandaa kwa baadhi ya matatizo haya utakayo kumbana nayo:

Usalama Wakati hatari zaidi kwa mwanamke ni baada ya kutoka. Mwanamume hana mamlaka juu yake na kwa kawaida hufanya lolote kupata mamlaka hayo. Anaweza kuendelea kukutishia kukuua. Mwanamke anastahili kuhakikisha anakaa mahala palipo salama ambapo mwanamume hajui au anapolindwa. Hastahili kumwambia mtu yeyote anapokaa. Kwani mtu huyo anaweza kulazimishwa kusema alipo.

Kujikimu mwenyewe Unahitaji kutafuta njia ya kujikimu na kuwakimu watoto wako. Ikiwa unaweza kukaa na marafiki au familia, tumia huo muda kupata elimu zaidi au kujifunza ustadi wa kazi. Ili kuhifadhi fedha, labda unaweza kuishi na mwanamke mwingine ambaye alidhulumiwa pia.


Hisia Mambo yote utakayohitaji kufanya kuanzisha maisha mapya yaweza kuonekana mengi kukabiliana nayo. Unaweza kuhisi hofu na upweke kwa sababu hujazoea kuishi pekee yako mahali pageni. Unaweza kumpeza mpenzi--haijalishi aliyokutendea. Wakati mambo yatakapo onekana kuwa magumu sana, unaweza kukosa kukumbuka jinsi mambo yalivyokuwa mabaya kabla ya kuondoka. Jipe muda wa kuhuzunika kuachana na mpenzi wako na maisha yako ya zamani. Jaribu kukaa imara. Ona kama unaweza kupata wanawake wengine wanaopitia hali sawa kama yako. Pamoja mnaweza kusaidiana.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020119